
Dr. Irene Kasalu anatarajiwa kuwa eneo la Mwingi wiki hii, katika ziara itakayolenga kuendeleza kampeni zake za ugavana na kuimarisha shughuli zake za kisiasa katika eneo hilo.
Katika ziara hiyo, Kasalu pia anatarajiwa kutoa mamilioni ya fedha kwa vikundi vya kina mama, huku akiendelea na mikutano na shughuli za maendeleo katika maeneo mbalimbali.
Kasalu pia amewakosoa wapinzani wake, akidai kuwa baadhi yao ni “wavivu”, huku wengine akiwatuhumu kwa ufisadi uliokithiri.
Ziara ya Mwingi inaongeza kasi katika harakati zake za kutafuta uungwaji mkono kuelekea uchaguzi wa ugavana.